Salim Kikeke "Nimedhalilishwa" |
Picha iliozagaa katika mtandao wa facebook, ikimwonyesha mtangazaji mashuhuri wa idhaa ya kiswahili ambae ni raia wa Tanzania; Salim Kikeke imezua mjadala mzito. Picha hiyo ambayo Kikeke aliipiga akiwa amesimama na mrembo ambae juzi alitwaa taji la miss dunia, imemsikitisha sana bwana Salim kikeke.
Akizungumza kwa njia ya simu toka Pemba, Tanzania (mapumzikoni) alisema anashangazwa sana na binadamu wenye akili fupi kumdhalilisha kiasi iko.Aliongeza kusema yeye ni baba wa watoto na anampenda na kumweshimu mke wake sana pia anapenda kupiga picha na watu maarufu duniani na hiyo sio mara yake ya kwanza. Ameshangazwa na aliyepost picha hiyo kumfanyia jambo la dharau kiasi hiki.
Alimalizia kusema yeye yote amemwachia mungu.
Source JF
SOMA ZIMEPIGWA BUNGENI KENYA, SPIKA AMWAGIWA SODA!!!!
0 Response to "SALIM KIKEKE WA BBC ASIKITISHWA KUDHALILISHWA MTANDAONI!!!!"
Post a Comment