ZA UKWELI SANA

ESCROW YALETA KIZAAZAA ZAIDI... TIBAIJUKA AGOMA KUJIUZULU.... JK AKATIZA ZIARA YA PINDA GHAFLA!!!!

Kizaazaa Serikalini
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, akiongea na wanahabari hivi punde ndani ya Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam amesema haoni sababu ya kujiuzulu kutokana na sakata la akaunti ya Escrow.
Aongeza kuwa watu wanaona suala la kujiuzulu kama fasheni ila yeye hayupo katika fasheni hiyo.
Wakati huo huo Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.
Pinda amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

0 Response to "ESCROW YALETA KIZAAZAA ZAIDI... TIBAIJUKA AGOMA KUJIUZULU.... JK AKATIZA ZIARA YA PINDA GHAFLA!!!!"

Post a Comment