ZA UKWELI SANA

CHAGUZI BALAA.... MGOMBEA UENYEKITI AFA GHAFLA MUDA MFUPI BAADA YA KUPIGA KURA!!!!!!!


Askari wakiwataka wananchi kutawanyika baada ya kuahirishwa uchaguzi wa Serikali za mitaa katika kituo cha Mabibo Mpakani Mtaa wa Jitegemee, Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao

Mgombea uenyekiti kupitia CCM Mtaa wa Swea, Kata ya Mkolani, Nyamagana, Mwanza, Pius Mihayo amefariki dunia ghafla akiwa mtaani kwake, muda mfupi baada ya kupiga kura. 
Msimamizi wa uchaguzi huo, Halifa Hida alisema mgombea huyo alifariki dunia ghafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea na chanzo cha kifo hicho hakijajulikana... “Sasa kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa viti maalumu, nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za uchaguzi zitakapoandaliwa,” alisema Hida.
ONA MATUKIO HAYA YA KUTISHA:
 

0 Response to "CHAGUZI BALAA.... MGOMBEA UENYEKITI AFA GHAFLA MUDA MFUPI BAADA YA KUPIGA KURA!!!!!!!"

Post a Comment