ZA UKWELI SANA

MUAGUAJI WA DIAMOND APIGWA KIFUNGO... YEYE AYEYUKA!!!!





Yule mganga aliyejitapa kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya amehukumiwa kifungo cha miaka saba (7) jela baada ya kukutwa na hatia katika kisa cha kuchanganya akihusishwa na wizi wa gari.

Hakimu Kisailo alitoa hukumu hiyo kwa maelezo kwamba, mnamo Januari 20, mwaka jana, maeneo ya Kariakoo jijini Dar, Yahya alidaiwa kuiba gari aina ya Toyota RAV4 lenye namba za usajili T 139 BSJ likiwa na thamani ya Sh. milioni 12, mali ya Edrick Elieza.

Wakati Hakimu Kisailo akisoma hukumu hiyo, mshtakiwa na wadhamini wake hawakuwepo mahakamani hapo hivyo alisema mara tu baada ya hukumu wahusika hao watakamatwa ili wakatumikie adhabu inayowakabili.
GPL.

0 Response to "MUAGUAJI WA DIAMOND APIGWA KIFUNGO... YEYE AYEYUKA!!!!"

Post a Comment