Yule mganga aliyejitapa
kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Ustadh Yahya amehukumiwa kifungo cha miaka saba (7) jela baada ya
kukutwa na hatia katika kisa cha kuchanganya akihusishwa na wizi wa gari.
Hakimu
Kisailo alitoa hukumu hiyo kwa maelezo kwamba, mnamo Januari 20, mwaka jana,
maeneo ya Kariakoo jijini Dar, Yahya alidaiwa kuiba gari aina ya Toyota RAV4
lenye namba za usajili T 139 BSJ likiwa na thamani ya Sh. milioni 12, mali ya
Edrick Elieza.
Wakati Hakimu Kisailo akisoma hukumu hiyo, mshtakiwa na
wadhamini wake hawakuwepo mahakamani hapo hivyo alisema mara tu baada ya hukumu
wahusika hao watakamatwa ili wakatumikie adhabu inayowakabili.
GPL.
GPL.